MWANADADA anayechipukia kwa kasi katika muziki wa kizazi kipya, Zena Muhamed ameweka wazi kuwa, hayupo tayari kufanya onyesho lolote bila ya kulipwa kitita cha sh. milioni tatu.
Zena, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la Shilole amesema yeye ni msanii maarufu hivyo hawezi kufanya onyesho kwa dau dogo.
“Mimi ni msanii mkubwa na ambaye anadhani kuwa nafanya shoo kwa dau dogo, imekula kwake. Anayetaka kunikodisha lazima ajipange,” alisema.
Shilole aliongeza kuwa, kwa mwaka huu amepania kuufanya muziki wake uwe wa kimataifa kwa vile anaamini anao wapenzi wengi nje ya nchi ambao wanapenda aina ya muziki anaopiga.
Katika hatua nyingine, mwanadada aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Njia panda’, Doreen Aurelian Cassian Ponera aka Pipi, ameamua kutoa picha za ujauzito wake.
Pipi, ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo mpya uitwao ‘Unapokuwa mbali’, ameyaondoa mashaka waliyokuwa nayo baadhi ya watu walioiona video hiyo na kugundua kuwa kuna mabadiliko kwenye saizi ya tumbo lake na hivyo kuhisi kuwa tayari ni mjamzito.
Kwenye ukurasa wake wa kuuzia sura 'Facebook' ameamua kuonyesha wazitumbo lake na kuwapa jibu wale walioukuwa na shaka na hali yake ya sasa.
No comments:
Post a Comment