'
Saturday, October 1, 2011
KUMRADHI NILIKWENDA BUTIAMA KIKAZI
Wapenzi wasomaji wa blogu hii ya liwazozito, kwa kipindi cha taktriban wiki moja sikuweza kupost chochote ndani ya blogu hii kwa sababu nilikuwa safarini katika kijiji cha Butiama kilichopo wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara kikazi. Nilipelekwa huko na mwajiri wangu kwa ajili ya kuandika makala za kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Safari hiyo pia ilinifikisha katika miji ya Mwanza na Mara. Pia nilipita katika wilaya za Bunda na Magu. Jiandaeni kusoma makala zenye mvuto kuhusu maisha ya Mwalimu Nyerere, mazingira ya kijiji chake cha Mwitongo pamoja na mahojiano niliyoyafanya na watoto wake na mdogo wake wa mwisho, mtoto pekee wa Chifu Nyerere aliyebaki hai hadi sasa. Pia mtasoma mengi kutoka kwa Chifu Wanzagi, ambaye aliachiwa usia mzito na Baba wa Taifa, siku chache kabla hajakwenda Uingereza kwa ajili ya matibabu. Je, unajua Baba wa Taifa alizungumza nini na Chifu Wanzagi?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment