KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, May 11, 2012

Eritrea yapata mrembo wa Afrika Mashariki

WAREMBO watakaoziwakilisha nchi zao katika mashindano ya mwaka huu ‘Miss East Africa’ wameanza kutangazwa.
Taarifa iliyotolewa na Kampuni ya Rena Events Ltd juzi ilisema kuwa, mrembo wa kwanza kupatikana ni Rahwa Afework (22) kutoka Eritrea.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mrembo huyo alipatikana hivi karibuni baada ya kuwabwaga warembo wenzake waliotaka kuiwakilisha Eritrea katika mashindano hayo.
Rahwa mwenye urefu wa mita 1.73, anasomea mambo ya ubunifu wa mitindo nchini Eritrea.
Fainali za mashindano hayo zimepangwa kufanyika Septemba 7 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
Nchi zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd ya Dar es salaam.
Wakati huo huo, shindano la kumsaka Miss Nyamagana 2012, linatarajiwa kufanyika Juni 2 mwaka huu kwenye ukumbi wa Gold Crest mjini Mwanza.
Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa shindano hilo jana ilisema kuwa, jumla ya warembo 25 wamejitokeza kuwania taji hilo, lakini orodha hiyo inaweza kuongezeka.



No comments:

Post a Comment