L OKWI AMWAIBISGA NCHUNGA
Simba leo ilisherehekea ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa staili ya aina yake baada ya kuibugiza Yanga mabao 5-0 katika moja ya mechi za mwisho za ligi kuu ya Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba ndiye aliyeibuka shujaa wa Msimbazi baada ya kufunga bao moja na kusababisha mabao mengine matatu.
Okwi alifunga bao la kwanza baada za mapema baada ya kuingia na mpira ndani ya 18 na kupiga shuti lililompima vyema kipa Yaw Berko na mpira kutinga wavuni.
Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu. Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mkangara alimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma baada ya timu ya Simba kuifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar salaam katika mchezo uliokuwa wa kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo.
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete