Hasheem Thabeet akiongea na waandishi wa habari (hawako pichani)
kuhusu kliniki ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Sprite itakayofanyika
katika viwanja vya Don Bosco, Upanga Dar es Salaam kuanzia Ijumaa Juni
Mosi 2012.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania
(TBF) Michael Maluwe akizungumza na waandishi wa habari (hawako
pichani)kuhusu ya kliniki ya vijanai chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika
katika viwanja vya Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia Ijumaa
Juni Mosi mwaka huu. Kliniki hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Coca-Cola
kupitia kinywaji cha Sprite. Katikati ni mchezaji wa Ligi maarufu duniani ya
NBA Hasheem Thabeet na kulia ni Meneja Bidhaa Msaidizi wa Coca-Cola
Tanzania Warda Kimaro.

Sprite, moja ya vinywaji maarufu vya kampuni ya Coca-Cola leo imetangaza
kudhamini kliniki ya mchezo wa kikapu kwa vijana chini ya umri wa miaka 17
itakayofanyika kwenye kiwanja cha Don Bosco, Upanga, jijini Dar es Salaam
kuanzia Ijumaa juni 1hadi June 2, chini ya mchezaji wa kimataifa wa mchezo
huo Hasheem Thabeet.
Zaidi ya vijana 200 kutoka mikoa sita watashiriki kliniki hiyo ambayo itatoa
mafunzo ya awali ya mchezo wa kikapu kama vile kumiliki mpira na kutoa
pasi. Katibu mkuu msaidizi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Michael
Maluwe amesema kuwa washiriki watatoka mikoa ya Mwanza, Mbeya,
Dodoma, Kilimanjaro, Arusha, Unguja na Pemba.
“Tunashukuru kupata fursa hii ya mafunzo ya awali kwa vijana ambao kusema
kweli ndiyo uti wa mungongo wa maendeleo ya mchezo wa kikapu hapa
Tanzania”, amesema Maluwe na kupongeza juhudi zinazofanywa na Coca-Cola
kupitia Sprite za kudhamini shughuli za maendeleo ya mchezo wa mpira wa
kikapu.
Hii ni mara ya pili kwa Sprite kudhamini kliniki ya kikapu kwa vijana chini ya
ukufunzi wa Hasheem Thabeet. Kliniki kama hii ilifanyika mwaka 2010 kwenye
uwanja huo huo wa Don Bosco na kushirikisha zaidi ya vijana 200 kutoka Dar
es Salaam na mikoa mengine.
Thabeet ni nembo ya mafanikio katika mchezo wa mpira wa kikapu na ni
mchezaji pekee kutoka Tanzania kuwahi kucheza kwenye ligi maarufu duniani
ya NBA. “Najisikia fahari kupata fursa kama hii, kwa mara nyingine tena, ili
kuweza kuwafundisha na kuwahamasisha vijana kucheza mpira wa kikapu.
Naamini baadhi yao watachomoza kuwa wachezaji nyota siku za usoni”,
alisema Thabeet ambaye yuko nchini tayari kuendesha kliniki hiyo.
Kwa upande wake, Meneja Mzaidizi Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Warda
Kimaro amesema: “Sprite inajisikia furaha kupata nafasi hii ya kusaidia
maendeleo ya mchezo wa kikapu na tunaamini kwamba kliniki hii ya Hasheem
Thabeet itawasaidia vijana kuelewa vitu msingi katika maendeleo ya mchezo
wa mpira wa kikapu”.
Sprite ilianza kudhamini mchezo wa mpira wa kikapu hapa nchini tangu
mwaka 2010 na tangia hapo imeweza kudhamini shughuli mbali mbali za
kikapu ikiwa ni pamoja na mashindano ya vijana mikoani, mashindano ya
kanda ya tano, mechi za timu ya Marekani AND1 ambao walikuwa hapa nchini
mwezi uliopita na kucheza mechi za kirafiki katika mikoa ya Mwanza, arusha
na Dar es Salaam kwa udhamini wa Sprite.
Mbali na kudhamini mashindano, Sprite pia imesaidia kuboresha viwanja wa
mchezo wa mpira wa kikapu katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Dodoma,
Mbeya, Mwanza, Arusha na Kilimanjaro.

No comments:
Post a Comment