KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, January 18, 2012

'Jokate dada yangu, Wema wa ubavu wangu'



SIKU chache baada ya kunusurika kufungwa jela mkoani Iringa, msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ’Diamond’ amebainisha kuwa, hana uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo na mrembo, Jokate Mwegelo.
Diamond alisema hayo wiki hii alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha radio nchini kuhusu kunusurika kwake kufungwa jela mkoani Iringa na hatma ya uhusiano wake wa kimapenzi na Wema Sepetu.
Alisema si kweli kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Jokate bali wamezoeana kama kaka na dada na ndio sababu ya kuwa karibu.
Msanii huyo alisema wa ubavu wake si mwingine zaidi ya Wema, ambaye tayari ameshamvisha pete ya uchumba na wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
Msimamo huo wa Diamond umekuja siku chache baada ya Jokate, mshindi wa tatu wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2008 naye kumkana msanii huyo.
Diamond pia alitumia fursa hiyo kuwaomba radhi Watanzania kutokana na tukio la kumshambulia mwandishi na mpiga picha wa mjini Iringa, Godwin Francis.
Tukio hilo lilitokea Desemba 31 mwaka jana kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa wakati Diamond na wacheza shoo wake wawili walipokuwa wakijiandaa kufanya onyesho.
Kufuatia tukio hilo, Diamond na wenzake hao walifunguliwa kesi na kufikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Iringa, ambapo walihukumiwa kifungo cha miezi sita jela ama kulipa faini ya sh. 80,000 kila mmoja. Washtakiwa hao walikiri kosa hilo na kulipa faini hiyo.

No comments:

Post a Comment