KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 12, 2012

Eucharia asimikwa kuwa mchungaji


LAGOS, Nigeria
BAADA ya kuokoka, hatimaye mcheza filamu nyota nchini Nigeria, Eucharia Anunobi amesimikwa kuwa mchungaji na kupewa jina la Mchungaji Easter.
Eucharia alisimikwa kuwa mchungaji Desemba 28 mwaka jana na baadhi ya wachungaji wenzake katika misa iliyofanyika kwenye kanisa la Fresh Oil Ministry lililopo Egbeda mjini Lagos.
Uamuzi wa msanii huyo kuokoka na hatimaye kusimikwa kuwa mchungaji, umepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wa sanaa ya filamu nchini Nigeria.
Kwa wanaomfahamu msanii huyo, wanamwelekezea kuwa, alikuwa mtu wa vitendo na mahiri katika ugizaji, hivyo uamuzi wake wa kuokoka unaonekana kama ni miujiza.
Baadhi ya marafiki zake wa karibu wamesema, wanashindwa kuelewa ni kwa nini Eucharia amefikia uamuzi huo, lakini wengine wamesema huenda ni kwa sababu ya kuguswa na neno la Mungu.
Hata hivyo, baadhi ya rafiki zake hao wamekaririwa wakisema kuwa, huenda uamuzi wake huo umetokana na hali ya mtoto wake, Raymond anayesumbuliwa na ugonjwa wa ‘sikoseli’.
Kabla ya kusimikwa kuwa mchungaji, Eucharia alikuwa muinjilisti na kuna habari kuwa, lengo lake la baadaye ni kufuata nyayo za wengine kwa kuanzisha kanisa lake binafsi. Eucharia ameshiriki kucheza filamu nyingi za Kinigeria na moja ya sifa zake zilikuwa kuvaa mavazi ya kubana na yaliyomtoa bomba.

No comments:

Post a Comment