KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, January 29, 2012

Twiga Stars yaichezesha kwata Namibia







TIMU ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars jana ilifuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika baada ya kuicharaza Namibia mabao 5-2 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yaliiwezesha Twiga Stars kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-2, kufuatia kuichapa Namibia mabao 2-0 katika mechi ya awali iliyochezwa mjini Whindhoek.

Mshambuliaji Mwanahamisi Omary ndiye aliyeibuka shujaa wa Twiga Stars baada ya kuifungia mabao matatu kati ya matano. Mwanahamisi alizawadiwa pesa nyingi na mashabiki.

Twiga Stars sasa itakutana na mshindi kati ya Misri na Ethiopia, ambazo zilitarajiwa kurudiana jana mjini Addis, Ababa. Katika mechi ya awali, Misri ilishinda mabao 4-2.

No comments:

Post a Comment