Azam ililazimika kumaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji 10 baada ya kiungo wake, Abdulrahim Humud kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 52 kwa kosa la kucheza rafu mbaya. Awali, Humud alikuwa ameonyeshwa kadi ya njano.
Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 35 lililofungwa na Danny Mrwanda kabla ya Azam kusawazisha dakika ya 45 kupitia kwa George Odhiambo.
Mechi hiyo ilikuwa ya pili kwa Simba na Azam. Katika mechi za kwanza, Simba iliichapa Mafunzo mabao 2-1 wakati Azam ilitoka sare ya bao 1-1 na Karume Boys.
Kwa matokeo hayo, Simba inaongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi nne baada ya kucheza mechi mbili sawa na Karume Boys, zikifuatiwa na Azam yenye pointi mbili. Mafunzo ni ya tatu ikiwa haina pointi.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo iliyochezwa jana, Karume Boys iliichapa Mafunzo bao 1-0. Bao pekee na la ushindi la Karume Boys lilifungwa na Nassor Matter dakika ya 45.
No comments:
Post a Comment