Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu amesema mjini Dar es Salaam leo kuwa, Niyonzima alirejea nchini juzi usiku kwa ndege akitokea Rwanda.
Sendeu alisema kuchelewa kwake kurejea nchini kulitokana na matatizo binafsi yaliyokuwa yamemkuta wakati akiwa nchini kwao.
Kwa mujibu wa Sendeu, mchezaji huyo amewataka wachezaji wenzake kurejesha heshima kwa mara nyingine kwa kutwaa kombe la Kagame katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Julai 14 Mwaka huu.
"Niyonzima amesema kwa muda wote aliokuwa mapunziko, amekuwa akifuatilia kwa karibu juu ya klabu yake ya Yanga, hasa katika zoezi la usajili unaoendelea na kupongeza usajili huo kutokana na baadhi ya wachezaji anaowafahamu kusajiliwa katika kikosi hicho,"alisema.
Yanga itaanza kutupa karata yake ya kwanza Julai 14 dhidi ya Atletico ya Burundi.
No comments:
Post a Comment