KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, June 22, 2012

Mwanza waomba kuandaa Kombe la Kagame

MKOA wa Mwanza umewasilisha maombi kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kuandaa michuano ya Kombe la Kagame, yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao mjini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, wameshayapokea maombi hayo na kuanza kuyafanyiakazi.
Kwa mujibu wa Wambura, wamekiomba chama hicho kiwasilishe bajeti yake ikiwa ni pamoja na kuonyesha uwezo wake wa kuzihudumia timu zitakapokuwa mkoani humo.
Wambura alisema iwapo maombi hayo yatakubaliwa, timu zitakazopangwa kituo cha Mwanza itabidi zisafirishwe kwa ndege kulingana na kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Iwapo ombi hilo litakubaliwa, itakuwa mara ya kwanza kwa michuano hiyo kufanyika Mwanza baada ya miaka mingi. Mara ya mwisho, michuano hiyo iliwahi kufanyika katika miji ya Morogoro na Arusha.

No comments:

Post a Comment