Kocha mpya wa Yanga, Marcio Maximo anatarajiwa kuwasili nchini wiki ijayo kwa ajili ay kuinoa timu hiyo kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kwa jina la Kagame cup.
Kocha huyo atawasili nchini pamoja na kocha msaidizi wa viungo. Pia katika msafara huo atakuwepo mke wake kutokana na ukweli kuwa Maximo hatakuwa na mpango wa kurejea kwao mpaka kumalizika kwa michuano ya Kagame.
Chanzo kutoka klabu ya Yanga kimesema kuwa Maximo amekubaliana na Yanga kwa ajili ya kuinoa timu hiyo na tayari ametoa mapendekezo kadhaa ya usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao.
Mapendekezo hayo ni pamoja na usajili wa wachezaji kadhaa kwa ajili ya kikosi chake na tayari klabu hiyo imekwisha kamilisha kwa asilimia kubwa. Wachezaji hao ni pamoja na kipa Ali Mustapha ‘Barthez’ na beki wa kati wa Simba, Kelvin Yondani ambaye amezua gumzo kubwa hapa jijini.
Mtoa habari amesema kuwa Barthez amekwisha saini mkataba wa klabu hiyo huku Yanga ikimtoa kwa mkopo kipa wake, Shaaban Kado kurejea timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.
Wachezaji wengine nyota waliosajiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ni beki wa timu ya Kagera Sugar, David Luhende, Mussa Hassan Mgosi kutoka timu ya DC Motema Pembe, Owen Kasule kutoka klabu ya Hoàng Anh Gia Lai Football Club ya Vietnam ambaye ni raia wa Uganda, Meddie Kagere (Polisi, Rwanda), Nizar Khalfan na Kelvin Yondani. Pia wamo akina Saidi Bahanuzi na Juma Abdul kutoka timu ya Mtibwa Sugar.
No comments:
Post a Comment