KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, August 3, 2012

KOZI YA UONGOZI FIFA KUANZA AGOSTI 6

Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) itafanyika Msimbazi Center jijini
Dar es Salaam kuanzia Agosti 6-11 mwaka huu ikiwa na
washiriki 30.
Washiriki wa kozi hiyo itakayonedeshwa na wakufunzi
kutoka FIFA ni viongozi kutoka TFF, Chama cha Mpira wa
Miguu Zanzibar (ZFA), vyama vya mpira wa miguu vya
mikoa, klabu za Ligi Kuu na viongozi wa mpira wa miguu
wa wanawake.
Walioteuliwa kushiriki ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa
TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu,
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi,
Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein
Mwamba na Eliud Mvella.
Wengine ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu
Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi),
Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
Makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya
Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri),
Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga
(Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo
Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.
Washiriki wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah,
Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa Habari,
Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio,
Jimmy Kabwe, Mkurugenzi wa Mashindano, Saad
Kawemba, Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa
wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina
Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa
zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.

No comments:

Post a Comment