KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, August 5, 2012

MANJI AVUNJA KAMATI ZOTE ZA YANGA

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji ametangaza kuvunja kamati zote za klabu hiyo zilizokuwepo katika uongozi uliopita chini ya mwenyekiti, Lloyd Nchunga.

Manji alitangaza kuvunja kamati hizo leo wakati akizungumza na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo katika makao makuu ya Yanga, mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

Uamuzi huo wa Manji umekuja muda mfupi baada ya yeye na viongozi wenzake wapya kula viapo vya uaminifu vya kuiongoza klabu hiyo mbele ya mdhamini mkuu wa klabu hiyo, Mama Fatume Karume.

Mbali na Manji, viongozi wengine waliokula viapo hivyo ni makamu mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wa kamati ya utendaji.

Hata hivyo, Manji alisema kamati pekee itakayoendelea na majukumu yake ndani ya Yanga ni ya uchaguzi inayoongozwa na Jaji John Mkwawa.

Manji alisema anatarajia kuunda kamati zingine mpya baada ya kikao cha kamati ya utendaji kinachotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment