KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, August 4, 2012

OKWI AMKARIBISHA NGASA SIMBA



Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Okwi amemkaribisha rasmi mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Mrisho Ngasa.
Okwi ametoa makaribisho hayo kwa Ngasa kupitia akaunti yake ya mtandao wa twitter leo.

Katika maelekezo yake ya kumkaribisha Ngasa, Okwi ameandika 'Welcome to Simba, Mrisho Ngasa, nguvu moja' , akiwa na maana 'Karibu Simba, Ngasa, nguvu moja'.

Ngasa amesajiliwa na Simba akitokea Azam baada ya kulipwa kitita cha sh. milioni 30 pamoja na gari.

Mshambuliaji huyo pia alikuwa akiwaniwa na klabu yake ya zamani ya Yanga, lakini vibopa wake walichemsha baada ya kudai kuwa, hana thamani, ambayo Azam ilikuwa ikitaka ilipwe ili imruhusu kuhama.

No comments:

Post a Comment