KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, August 4, 2012

DOGO JANJA ATAMANI KUKUTANA NA MADEE

Msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Dogo Janja amesema anatamani kukutana na mlezi wake wa zamani, Madee wa kundi la Tip Top Connection.

Akihojiwa katika kipindi cha Amplifier cha Clouds FM, Dogo Janja amesema tangu aliporejea Dar es Salaam kutoka kwao Arusha, hajabahatika kukutana na Madee.

Msanii huyo mahiri kwa kuchana amesema, mwanzoni hakuwa akitaka kukutana na Madee kwa sababu ya hasira alizokuwa nazo, lakini kwa wakati huu anatamani kumuona.

Madee ndiye aliyevumbua kipaji cha Dogo Janja miaka minne iliyopita na kumuhamishia mjini Dar es Salaam na kumtafutia shule katika sekondari ya Jitegemee.

Akiwa Tip Top, Dogo Janja alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na tungo zake na kupata ofa nyingi za kufanya maonyesho.

Hata hivyo, uhusiano wa dogo huyo na Madee ulianza kuyumba na hatimaye kukorofishana kabla ya Madee kuamua kumrejesha chalii huyo kwao Arusha kwa madai kuwa, alikuwa hataki shule na alijikita zaidi katika anasa.

Lakini Dogo Janja alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa, Madee alikuwa akimtumia kupata pesa na kwamba kwa kipindi chote alichokuwa Tip Top hajawahi kunufaika na kipaji chake zaidi ya kuambulia visenti vichache.

Kwa sasa, Dogo Janja yupo katika kundi la Mtanashati linalomilikiwa na mfanyabiashara, Ustaadh Juma Namusoma na tayari ameshaibuka na kibao kipya.

Singo hiyo ni ya kwanza kuirekodi toka ameondoka kwenye kundi la TipTop Connection June 13 2012 na imerekodiwa kwa Marco Chali, MJ Records ambapo PNC amepewa shavu kwenye chorus. Ni singo inayozungumzia maisha ya ukweli ya Dogo Janja.

No comments:

Post a Comment