Didier Kavumbangu, mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Atletico Olympique ya Burundi, alikuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya sita baada ya kupiga mpira ambao beki alipojaribu kuokoa ulimgonga kipa wake na kuingia nyavuni.Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0.
Kipindi cha pili, Haruna Niyonzima aliifungia Yanga bao la pili kwa penalti dakika ya 57, baada ya Simon Msuva kuchezewa rafu na Semmy Kessy kwenye eneo la hatari
Frank Damayo aliyeingia kuchukua nafasi ya Athumani Iddi ‘Chuji’ kipindi cha pili alitoa pasi nzuri kwa Simon Msuva ambaye aliifungia Yanga bao la tatu dakika ya 72, kabla ya Jerry Tegete kufunga la nne dakika ya 90+1.

Baada ya mchezo huu, Yanga ambao ni mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Jumatano kwenda Kigali, Rwanda ambako itaweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu.
Ikiwa huko, Yanga itacheza mechi kadhaa za kujipima nguvu na vigogo wa Rwanda, kama APR, Rayon, Atracao na Polisi kabla ya kurejea Dar ves Salaam kuanza maandalizi ya Ligi Kuu.
CHANZO CHA GABARI: BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment