KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, August 5, 2012

MAMA KARUME AWAAPISHA VIONGOZI WAPYA YANGA

Mama Karume akiwasili makao makuu ya klabu ya Yanga na kupokewa na mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo, Francis Kifukwe (kulia). Kushoto ni Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu.

Mama Karume akiongozwa kuingia kwenye jengo la Yanga. Kulia ni Mwenyekiti wa baraza la wazee, Jabir Katundu na kushoto ni mjumbe wa kamati ya utendaji, Musa Katabalo.

Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuf Manji (kulia) akiteta jambo na mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo, Francis Kifukwe.

Ni wakati wa kuomba dua. Hafla hiyo ilianza kwa viongozi na wanachama kusoma dua

Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa akifungua hafla ya uapishaji wa viongozi wapya

Yanga Oyee! Ndivyo anavyoelekea kusema Mama Karume kabla ya kuwaapisha viongozi wapya wa Yanga.

Tunatakiwa kushikamana na kuwa wamoja. Ndivyo alivyosema Mama Karume wakati akizungumza na viongozi wapya wa Yanga kabla ya kuwaapisha.


Mama Fatume Karume akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa huku Mzee Jabir Katundu akiwasikiliza.

Mzee Jabir Katundu akimuongoza Mussa Katabalo kula kiapo cha uaminifu cha kuitumikia Yanga

Yussuf Manji akila kiapo akiongozwa na Mzee Jabir Katundu

Mama Fatuma Karume akimpongeza Manji baada ya kula kiapo


Mama Karume akiwa na viongozi wapya wa Yanga baada ya kuapishwa


Kijana mi nakwenda, kazi kwako, sitaki kusikia mambo yanakwenda mrama. Ndivyo Mama Karume alivyokuwa akimueleza Manji wakati wakiagana. (Picha zote na Emmanuel Ndege wa blogu ya liwazozito)

No comments:

Post a Comment