KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, August 3, 2012

BINGWA MICHUANO YA BANCABC SUPER 8 KUZOA MIL 40/-

Bingwa wa michuano ya BancABC Super 8 inayoanza
keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) katika miji ya Dar es
Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata sh. milioni
40.
Mshindi wa pili wa michuano hiyo atapata sh. milioni 20.
Pia timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja

itapata sh. milioni 15 wakati zilizobaki kila moja itapata

sh. milioni 5.
Timu zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi
A lina timu za Simba (mabingwa wa Tanzania Bara),
Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za Zanzibar. Kundi B ni
Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa
Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.
Mechi za ufunguzi keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni
Simba vs Jamhuri (Dar es Salaam), Zimamoto vs Mtende
(Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro (Arusha) na
Super Falcon vs Azam (Zanzibar).

Awali mashindano yalikuwa yaanze Agosti 4 mwaka huu

lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja.
Hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi
za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam.
Nimeambatanisha ratiba.
Mdhamini bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa
timu zote kutoka kituo kimoja hadi kingine, malazi na jezi.
Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na nafasi yake
imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya
nne kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

No comments:

Post a Comment