KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, August 3, 2012

NGASA APEWA JEZI NAMBA 16 SIMBA

MCHEZAJI mpya wa Simba, Mrisho Ngassa, leo
amekabidhiwa jezi namba 16 atakayokuwa akiitumia
kwenye klabu yake msimu huu.
Ngassa alikabidhiwa jezi yake hiyo katika makao makuu ya
Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu
Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.
Kaburu alisema Simba inamkaribisha Ngassa kwa moyo
mmoja na kwamba wapenzi wote wa Wekundu wa
Msimbazi wana imani kubwa naye kwani uwezo wake
mkubwa wa soka unafahamika ndani na nje ya nchi.
"Tunashukuru kwamba tumekidhi vigezo vyote
vilivyohitajika kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyu.
Tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya
kumaliza muda wa mkopo wake kutoka Azam na ni imani
yetu kwamba ujio wa Ngasa utaimarisha zaidi timu kwani
yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa
Simba, Milovan Cirkovic, anawapenda," alisema.
Akizungumza katika tukio hilo, Ngassa alisema amefurahi
kusajiliwa na Simba kwani ni sawa na historia kujirudia,
akikumbusha kwamba baba yake mzazi, Khlfan Ngassa,
aliwahi kuwa mchezaji wa klabu katika miaka ya 1990.
Kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ngassa
alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba katika
ufukwe wa Coco, jijini Dar es Salaam ambako Simba
inaendelea na mazoezi yake chini ya makocha Amatre
Richard na James Kisaka.

MAANDALIZI MKUTANO MKUU YAENDA VIZURI

MKUTANO Mkuu wa Wanachama Wote wa Simba
utafanyika Agosti tano mwaka huu katika Bwalo la Maofisa
wa Polisi Oysterbay kama ilivyopangwa.
Mipango yote kwa ajili ya mkutano huo muhimu kikatiba
imekamilika na klabu inawaomba wanachama wake wote
hai kuhudhuria mkutano huo muhimu.
Uongozi umepanga kutoa mabasi kwa ajili ya
kuwasafirisha wanachama wake kutoka katika maeneo
mbalimbali kwenda katika ukumbi wa mikutano.
Kutakuwa na mabasi matatu kwenye eneo la Shibam
Magomeni... Mabasi matatu Temeke mwisho na mabasi
matatu katika makao makuu ya Simba SC Mtaa wa
Msimbazi.
Pia klabu itapeleka mabasi mawili katika wilaya za
Mkuranga na Kibaha kwa ajili ya kuwaleta wanachama
wake walio katika mkoa wa Pwani kuhudhuria mkutano
huo.
Mwenyekiti wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage,
amewahakikishia wanachama wa Simba kwamba mkutano
huo utaendeshwa kisasa na usalama umehakikishwa kwa
asilimia 100 kwa vile eneo la mkutano liko chini ya Jeshi la
Polisi.
"Napenda kuwahakikishia wanachama wote wa Simba
kwamba mkutano huo utakuwa bora na wote watakaokuja
watafurahi na kujisikia fahari kuwa washabiki wa klabu ya
soka ya Simba.

"Kwa wale ambao wamepanga kuja kufanya
vurugu kwenye mkutano huo, klabu itaviachia vyombo vya
dola vifanye kazi yake," alisema.

No comments:

Post a Comment