BAADA ya ukimya wa muda mrefu, msanii Ally Ramadhani, maarufu kwa jina la AT ameibuka na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Vifuu Tundu’.
AT amerekodi kibao hicho kwa kutumia swaga za mduara na inasemekana ameamua kuwapiga dongo wasanii wenzake wa kundi la Offside Trick lenye maskani yake Zanzibar.
Akizungumza mjini hapa mwanzoni mwa wiki hii, AT alisema ameamua kuwapiga madongo wasanii wa kundi hilo kwa lengo la kulipiza kisasi.
Alidai kuwa, kundi hilo hivi karibuni lilirekodi kibao cha ‘Kidudu mtu’ kwa lengo la kumkashifu yeye hivyo naye ameamua kulipiza kisasi.
“Nimeamua kuwaonyesha kuwa mimi ni mkali wa kutunga mashairi ya kupiga madongo kuliko wao, nadhani hili litakuwa fundisho kwa ‘wajinga’ wengine wanaopenda kutumia majina ya watu kutafuta umaarufu,” alisema AT.
Msanii huyo mwenye maskani yake Zenj alianza kupata umaarufu kimuziki alipoibuka na kibao chake cha ‘Nipigie’, alichomshirikisha mkongwe Stara Thomas.
AT pia aling’ara katika kibao cha ‘Mama ntilie’ kilichotungwa na Gelly, aliyemshirikisha pia mwanadada Rehema Chalamika ‘Ray C’.

No comments:
Post a Comment