KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, May 8, 2011

Man United bingwa 99%

MANCHESTER United jana ilijiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England baada ya kuibwaga Chelsea mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.
Ushindi huo uliiwezesha Manchester United kuongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi sita kati yake na Chelsea huku ikiwa imesaliwa na mechi mbili mkononi.
Baada ya matokeo ya mechi za jana, Manchester United sasa inazo pointi 76 baada ya kucheza mechi 36, ikifuatiwa na Chelsea yenye pointi 70 na Arsenal yenye pointi 67.
Bao la kwanza la Manchester United lilifungwa na Javier Hernandez baada ya gonga safi kati ya Ryan Giggs na Park Ji-Sung, aliyetoa pasi kwa mfungaji.
Beki Nemanja Vidic aliiongezea Manchester United bao la pili baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi iliyochongwa na Giggs, aliyegongewa kona fupi. Mabao hayo yalidumu hadi mapumziko
Bao la kujifariji la Chelsea lilifungwa na kiungo Frank Lampard baada ya Ramires kugongeana pasi murua na Branislav Ivanovic, aliyetoa pasi kwa mfungaji.
Wakati huo huo, matumaini ya Arsenal kutwaa taji hilo yamezidi kuyeyuka baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Stoke City katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa mjini hapa.
Mabao ya Stoke yalifungwa na Kenwyne Jones na Jermaine Pennant kipindi cha kwanza na Johan Djourou katika kipindi cha pili. Bao la kujifariji la Arsenal lilifungwa na Robin van Persie.



KIUNGO Florent Malouda (kushoto) wa Chelsea akiruka hewani kupiga mpira kwa kichwa huku akiwa amezongwa na beki Fabio Da Silva wa Manchester United, timu hizo zilipomenyana jana katika mechi ya ligi kuu ya England iliyochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford. Manchester United ilishinda mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment