KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, May 12, 2011

Kocha Bafana Bafana aihofia Taifa Stars

Pitso Mosimane



KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana, Pitso Mosimane amesema anaiheshimu na kuihofia timu ya Taifa, Taifa Stars.
Pitso aliueleza mtandao wa Goal wiki hii kuwa, anaamini Taifa Stars itatoa upinzani mkali kwa Bafana Bafana, timu hizo zitakapomenyana keshokutwa.
“Ni timu ngumu na wanashika nafasi ya pili kwenye kundi lao katika michuano ya kuwania kufuzu fainali za Afroka 2012 na walipata sare ugenini dhidi ya Algeria,”alisema kocha huyo.
“Nina furaha kwamba watawaita wachezaji wao watatu wanaocheza soka ya kulipwa nje. Itakuwa kipimo kizuri kwetu,”aliongeza.
Kikosi cha Bafana Bafana kinatarajiwa kuwasili nchini leo, kikiongozwa na kiungo wa klabu ya Kaizer Chiefs, Siphiwe Tshabalala.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, kikosi hicho kinatarajiwa kuwasili saa 1.30 usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.
Pambano kati ya Taifa Stars na Bafana Bafana limepangwa kuanza saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wengine waliomo kwenye kikosi hicho ni makipa Itumeleng Khune na Wayne Sandilands. Mabeki ni Morgan Gould, Siyanda Xulu, Eric Matoho, Mzivukile Tom, Prince Hlela, Siyabonga Sangweni, Tefu Mashamaite na Siyanda Zwane.
Viungo ni Hlompho Kekana, Thanduyise Khuboni, Reneilwe Letsholonyane, Thandani Ntshumayelo,Thabo Matlaba, Erwin Isaacs na Sifiso Myeni wakati washambuliaji ni Bernard Parker, Vuyisile Wana, Lehlohonolo Majoro na Katlego Mphela.
Kocha Pitso ameshindwa kuwaita wachezaji wake wanaocheza soka ya kulipwa nje kutokana na kuzuiwa na klabu zao. Baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na Bernard Parker, anayecheza Ugiriki.
Wakati huo huo, Wambura amesema klabu ya Vancouver Whitecaps imemnyima ruhusa kiungo, Nizar Khalfan kwa vile wiki ijayo timu hiyo itakuwa na mechi muhimu ya ligi.
Wambura alisema ujio wa wachezaji Idrissa Rajab, Henry Joseph, Abdi Kassim, Dan Mrwanda na Athuman Machupa bado wanafuatilia majibu katika klabu zao.

No comments:

Post a Comment