Hatua hiyo inafuatia jana, klabu ya Yanga kupitia msemaji wake Louis Sendeu kuweka wazi kuwa wamemsainisha mkataba wa mwaka mmoja nyota huyo ukiwa na thamani y ash.milioni 30.
Pamoja na dau hilo, Yondan pia atakuwa akilipwa mshahara wa shilingi 800,000 kila mwezi pamoja na stahili nyingine.
Sendeu alisema wameamua kumsajili Yondan kutokana na ukweli kwamba mkataba wa nyota huyo ndani ya klabu ya Simba umemalizika tangu mwanzoni mwa mwezi Mei huku ule wa Yanga aliousaini Februari 20 utamalizika Machi 20, 2013.
Aliongeza kuwa wamefuata taratibu zote zinazostahili kwa mujibu wa kanuni na sheria za Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA) ikiwemo kufanya naye mazungumzo kabla ya miezi sita.
Sendeu aliongeza kuwa hawatoyumba katika hilo na hasa vitisho kutoka kwa viongozi wa Simba ambao hivi karibuni wamekuwa wakizungumzia suala hilo.
Wakati Sendeu akisema hilo, Simba kupitia kwa mwenyekiti wake Ismail Aden Rage alisisitiza kuwa Yondan ni mchezaji wao halali na atakayemsajili atakwnda na maji.
Yondan anaingia katika historia nyingine ya vilabu za Simba na Yanga kuingia katika ushindani wa kuingiliana wachezaji wake ambapo iliwahi kutokea kwa Victor Costa, Kenneth Assamoh,Amri Said, Mohammed Mwameja Kenneth Mkapa na Athuman Iddy ‘Chuji’
No comments:
Post a Comment