Abdalla Ahmad Bin Kleb
Yono Kevela
Mussa Katabalo
WAGOMBEA 33 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga unaotarajiwa kufanyika Julai 15 mwaka huu.
Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili alisema jana kuwa, kati ya wagombea hao, 29 walirejesha fomu wakati wanne walishindwa kuzirejesha.
Aliwataja wagombea waliojitokeza kuwania nafasi ya mwenyekiti kuwa ni Yussuf Manji, John Jambele, Edgar Chibula na Sarah Ramadhani. Fomu ya Manji ilirejeshwa na mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji, Abdalla Ahmad Bin Kleb.
Aliwataja waliojitokeza kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti kuwa ni Ayoub Nyenzi, Yono Kevela, Ally Mayay na Clement Sanga.
Wanachama waliojitokeza kuwania nafasi ya ujumbe ni Bin Kleb, Mussa Katabalo, Lameck Nyambaya, Edgar Fongo, Ahmad Waziri Gao, Jumanne Mwamenywa, Peter Haule, Gaudius Ishengoma, Abdalla Sharia, Ramadhani Kampira, Mohamed Mbaraka, Ramadhani Saidi, George Manyama, Aron Nyanda, Omar Ndula, Shaaban Katwila, Justine Baruti na Jamal Kisongo.
Wagombea walioshindwa kurejesha fomu zao ni Eliakhim Masu, Muzamil Katunzi, Muhingo Rweyemamu na Isaac Chanja.
Uchaguzi mkuu wa Yanga umeitishwa baada ya mwenyekiti wa zamani, Lloyd Nchunga, makamu wake, Davis Mosha na wajumbe watano wa kamati ya utendaji kutangaza kujiuzulu kutokana na sababu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment