LAGOS, Nigeria
LICHA ya kufunga ndoa hivi karibuni, imeelezwa kuwa mcheza filamu machachari wa Nigeria, Ini Edo anaongoza katika orodha ya waigizaji tishio wa kike kwa ndoa za watu.
Utafiti uliofanywa na mtandao wa naijerules hivi karibuni umebaini kuwa, Ini amekuwa tishio zaidi kwa ndoa za watu kutokana na uzuri wa sura na umbile lake.
Ini ndiye mwigizaji tajiri wa kike wa filamu nchini Nigeria, akifuatiwa na Rita Dominick, Uche Jombo na Genevieve Nnaji.
Ini, mzaliwa wa Akwa Iborn amejipatia umaarufu mkubwa nchini Nigeria kutokana na uigizaji wake maridhawa katika filamu mbalimbali.
Mbali na kulipwa pesa nyingi kutokana na uigizaji filamu, Ini pia amekuwa akiingizia pesa nyingi kutokana na kuwa na mikataba ya kutangaza bidhaa mbalimbali.
Japokuwa kwa sasa Ini yupo kwenye ndoa, wanawake wengi wa Nigeria bado wanamuona kuwa tishio katika ndoa zao kwa vile wanaume wengi wamekuwa wakimpapatikia.
Kabla ya kuolewa, Ini alikuwa akihusishwa na migogoro mingi ya ndoa zilizovunjika, akiwemo kigogo mmoja, ambaye alilazimika kuvunja ndoa yake na kutangaza kumuoa mwanadada huyo mwenye macho yenye mvuto.
Ini ameelezewa kuwa ni mwanamke mwenye uwezo wa kumpata mwanaume yeyote anayemuhitaji. Kwa sasa, Ini amefunga ndoa na Philips Ehiagwina, mmarekani anayeishi Nigeria. Philips ameamua kufunga ndoa na Ini baada ya kuachana na mkewe, Ruth Okoro, ambaye alisota naye kimaisha kwa miaka mingi. Waigizaji wengine wa kike waliotajwa kuwa tishio kwa ndoa za watu ni Oby Edozien, Benita Nzeribe, Lola Alao, Anita Joseph, Grace Amah na Nkiru Sylvanus
No comments:
Post a Comment