KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, March 4, 2011

Nimechoka kuzaa watoto- 2 Face

LAGOS, Nigeria
MWANAMUZIKI nyota wa Nigeria, Tuface Idibia amesema amechoka kuzaa watoto, japokuwa hajafunga ndoa na mwanamke yeyote miongoni mwa wapenzi wake.
Akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa maziwa ya New Milo zilizofanyika mjini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita, Tuface alisema hataki kumpa mimba mwanamke mwingine yoyote.
Tuface, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, alisema hayo mbele ya wanafunzi na mama zao, waliohudhuria sherehe hizo zilizofanyika kwenye Jumba la Taifa la Sanaa la Iganmu.
“Sitaki kumpa mimba msichana yoyote zaidi,”alisema mwanamuziki huyo kwa kiingereza chenye lafudhi ya Kimarekani. Mwanamuziki huyo, ambaye tayari ameshazaa watoto watano kutoka kwa wanawake watatu tofauti, aliwaeleza watu waliohudhuria sherehe hizo kwamba ni vizuri kujifunza kutokana na makosa.
Wanawake waliozaa na mwanamuziki huyo ni Pero, Sumbo na Ann Macaulay.
“Hamuwezi kuelewa hisia nilizonazo sasa. Natamani ningekuwa na umri wa miaka 15 kama mlivyo nyinyi, hapo mtaelewa hisia zangu,”alisema.
Katika sherehe hizo, Tuface aliimba wimbo wa kumpongeza Gavana wa Jimbo la Lagos, Babatunde Raji Fashola na kuwashauri wanasiasa wengine kuyaongoza vyema majimbo yao. Naye mke wa gavana huyo, Abimbola Fashola aliwataka akinamama kuwa karibu na watoto wao ili iwe rahisi kwao kugundua vipaji vyao tangu wakiwa wadogo.

No comments:

Post a Comment