KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, March 21, 2011

WASANII 13 WA FIVE STARS WAFARIKI KATIKA AJALI

ISSA KIJOTI, mmoja wa waimbaji wa kikundi cha taarab cha Five Stars, anayedaiwa kufariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jana usiku mjini Morogoro.

BAADHI ya wasanii wa kikundi cha taarab cha Five Stars, ambao inadaiwa walifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jana usiku mjini Morogoro.

Wanamuziki 13 wa kundi la Five Stars Modern Taarab, 'Watoto wa Bongo' wamefariki dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Mikumi mkoani Morogoro. Katika ajali hiyo, wasanii 12 walifariki papo hapo, akiwemo muimbaji maarufu wa kundi hilo Issa Kijoti.
Taarifa zinasema ajali hiyo imetokea baada ya gari lililokuwa limewabeba wanamuziki wa kundi la taarab la Five Stars kugongana uso kwa uso na roli la mbao, wakati wakitokea mikoani kurejea Dar es Salaam.
Waliotambuliwa kufariki dunia mpaka sasa ni pamoja na Issa Kijoti, Hamisa Omary, Husna Mapande, Omary Hashim, Nasor, Sheba Juma, Tizo Mkunda na Samir Maulid.
Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, tayari miili ya marehemu hao imeondolewa eneo la ajali na kupelekwa katika hospitali ya mkoa ya Morogoro.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Morogoro jana, kiongozi wa kundi hilo, Ally J alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Walionusurika katika ajali hiyo ya kusikitisha ni pamoja na muimbaji mkongwe, Mwanahawa Ally, ambaye alikuwa kama muimbaji mualikwa katika ziara hiyo.
Mbali na Mwanahawa, rais wa bendi hiyo Ally J naye amenusurika katika ajali hiyo wakati
waimbaji wengine nyota, Jokha Kassim na Issa Kamongi hawakusafiri na kundi hilo katika safari hiyo.
Kundi hilo lenye upinzani mkali na Jahazi, liliondoka Dar es Salaam wiki iliyopita kwenda katika
katika mikoa ya Morogoro, Singida na Mbeya kwa ajili ya kufanya maonyesho na kutambulisha albamu zao walizozizindua mwanzoni mwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment