KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, May 11, 2014

MANJI AAHIDI KUFANYA USAJILI WA NGUVU YANGA



MWENYEKITI wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Yussuf Mehboob Manji amesema kwamba atafanya usajili wa kutisha na pia ahadi yake ya kujenga Uwanja wa kisasa katika klabu hiyo ipo pale pale.


Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu leo, Manji amesema yameongelewa mengi sana kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao hakuwepo nchini kwa ajili ya kazi zake binafsi lakini sasa amerejea na maandalizi ya msimu ujao yameshaanza.

Aidha, Manji amesema kwamba kuondoka kwa wachezaji wao wawili Didier Kavumbagu na Frank Domayo sio mwisho wa timu, kwani uongozi wake unaendelea na mipango ya kuhakikisha inasajli wachezaji wengine wazuri ambao wataisadia timu kwenye msimu ujao kwa kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi.

“Kuondoka kwa Kavumbagu ni kutokana na kuchelewa kwa majibu ya TFF juu ya idadi ya wachezaji wageni kwa msimu mpya, huku Domayo ambaye tangu mwaka jana aliombwa kuongeza mkataba alikua akisema anamsubiria mjomba wake ndipo aweze kufanya hivyo,”.

Amesema pamoja na kuondoka kwa wachezaji hao bado kwa kushirikiana na aliyekuwa kocha wao, Hans van der Pluijm watahakikisha Yanga inaendelea kutisha msimu ujao na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.

Hans aliahidi kuleta wachezaji wazuri watakaoisaidia Yanga siku alipokua akiiongea na waandishi wa habari kuwaaga.

Aidha Manji amelifuta rasmi tawi la Tandale kutokana na kuwa na chanzo cha vurugu na migogoro ndani ya klabu, pia amewafuta uanachama wanachama sita ambao walikiuka katiba ya Yanga kwa kwenda kuongea na waandishi na HABARI bila ya Idhini ya uongozi huku pia wakishindwa kulipia ada zao za uanachama kwa zaidi ya miezi sita.

Waliofutwa uanachama ni Ally Kamtande, Isihaka Dude, Hamisi Matandula, Waziri Jitu Ramadhani, Mohamed Kigali Ndimba na Selaman Hassan Migali.

Amekumbushia mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba utafanyika terehe mosi Juni, 2014 katika Ukumbi wa Oysterbay Police Mess na wanachama wote wanaombwa kulipia ada zao ili waweze kuhuhudhira mkutano huo wakiwa hai.

Manji amesema suala la ujenzi wa Uwanja wa Kisasa eneo la Jangwani bado lipo pale pale, kikubwa kinachosubirwa ni majibu ya serikali juu ya maombi ya eneo la ziada, kwani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema suala hilo lipo ukingoni na mda si mrefu.

No comments:

Post a Comment