'
Sunday, May 11, 2014
HANS AAGA YANGA, AOMBA UANACHAMA
Katibu Mkuu wa Yanga SC, Beno Njovu (kushoto) akiongea na wandishi wa habari, kulia ni aliyekua kocha mkuu wa Yanga Hans Van der Pluim
Hans Van Der Pluijm kocha mkuu wa timu ya Young Africans leo amewaaga rasmi wachezaji wake, viongozi, wapenzi na wanachama baada ya kumalizaa wake wa miezi sita na sasa anakwenda kujiunga na timu Al Shoalah FC iliyopo Ligi Kuu nchini Saudi Arabia.
Kocha huyo mdachi ambaye ameiongoza Young Africans kwa kipindi cha miezi mitano amesema anashukuru kwa sapoti aliyokua akiipata kutoka kwa wachezaji, viongozi, wapenzi na wanachama wa timu hii kwa kipindi chote alipokuwa nchini Tanzania.
"Najua wengi itawashangaza kuona naondoka lakini ukweli ni kwamba niikua na hiyo deal hata hata kabla ya kuja Yanga, nilikua na makubaliano na timu ya Al Shoalah FCmakubaliano ambayo yanaanza mwezi ujao hivyo nilikubaliana na viongozi wa Yanga kuja kufanya kazi kwa kipindi cha miezi sita tu, nashukuru tumefanya kazi salama na baada ya mkataba huo kuisha nipo tayari kurudi kuja kufanya kazi Tanzania" alisema Hans
Naipenda Yanga SC, nimejaza fomu kuomba uanachama hivyo mimi ni sehemu ya Yanga na katika usajili ujao nitawasaidia kuleta wachezaji wazuri ambao wataisaidia timu kwenye msimu ujao kwa Ligi ya Vodacom na mashindao ya Kimataifa.
Kocha Hans anaondoka leo nakwenda Ghana kisha baadae atakwenda nchini Saudu Arabia tayari kwa kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao katika timu yangu hiyo ambayo nitaitumikia kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kuhusu usajili kocha mkuu ameshakabidhi ripoti yake ya kiufundi jana, viongozi wanaifanyia kazi kisha baadae itawekwa wazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment