KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, May 6, 2014

RED CROSS KUTETA NA TFF



NA SOLOMON MWANSELE,MBEYA.


CHAMA Cha Msalaba Mwekundu Tanzania, kimesema kinataka kuzungumza na uongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), ili kuweza kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwenye viwanja mbalimbali vya soka.

Imeelezwa wamefikia hatua hiyo kutokana na kuwa TFF wamekuwa ni mojawapo ya wadau ambao wanasababisha mikusanyiko mikubwa ya watu wanaojitokeza kushuhudia michezo mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Rais wa Chama hicho nchini,Dk.George Nangale, aliyayasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika viwanja hoteli ya Mbeya Paradise Inn, iliyopo jijini Mbeya.

Dk.Nangale alisema Chama hicho kinahitaji msaada kutoka TFF ili kiweze kufanya kazi zake za kutoa huduma kwa wachezaji wanaoumia viwanjani kwa ufanisi zaidi, kuliko ilivyo sasa hivi.

Aliongeza lengo la kukutana na uongozi wa TFF chini ya Rais wake,Jamali Malinzi, ni kuhakikisha kunakuwepo utaratibu mzuri unaoeleweka kati ya Chama hicho na Shirikisho hilo la Soka.

“Mbali ya TFF pia tunataka kuwa kushirikiana kwa karibu zaidi na vyama vya siasa nchini,kwani navyo vinapelekea mikusanyiko mikubwa kwenye mikutano yao ya hadhara” alisema Dk.Nangale.

Alisema Chama hicho kinao wataalamu wa kutosha katika masuala ya utoaji huduma katika matukio, hivyo wanatarajia kuwa mazungumzo yao kati ya TFF na vyama vya siasa yataenda vizuri.

Dk.Nangale alisema wanataka walau wawe na mahema maalumu, viwanjani ambapo wachezaji wakiumia watakuwa wanahudumiwa humo na kama tatizo linakuwa kubwa zaidi basi ndipo wakimbizwe hospitalini kwa huduma zaidi.

No comments:

Post a Comment