KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, May 11, 2014

MABADILIKO YA KATIBA YANGA JUNI MOSI

Uongozi wa klabu ya Young Africans Sports Club umeitisha mkutano mkuu wa wanachama wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama waweze kutoa maamuzi kwenye baadhi ya vipengele vilivyoongezwa kabla ya kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa viongozi.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani, Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema wamefikia kuitisha mkutano huo wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama wapate fursa ya kupitisha baadhi ya vipengele kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

"Tumekua na mawasiliano na TFF juu ya kuongezwa baadhi ya vipengele kwenye Katiba yetu kabla ya kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi, baada ya hapo ni nafasi kwa wanachama wa Yanga sasa kukutana na kuweza kupitisha hivyo vipengele vitakavyoongezwa kwenye Katiba Mpya" alsiema Beno.

Aidha Beno amesema wanachama wakishapitisha/kukubaliana juu ya hivyo vipengele ndipo uoungozi utawasilisha mapendekezo hayo kwa TFF ambayo ikishayabariki, yatapelekewa kwa Msajili nae akiyapitisha ndipo itakua tayari ni Katiba halali ambayo itatumika kwwenye uchaguzi mkuu.

"Nawaomba wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano wa mabadiliko juni mosi 2014 ili waweze kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea kuwa na Katiba Mpya itakayotumika kwa shughuli za kila siku za klabu ya Yanga SC" aliongea Beno.

Eneo na Ukumbi utakapofanyika mkutano huo Juni Mosi 2014 utatangazwa hivi karibuni mara baada ya taratibu zote kukamilika.

No comments:

Post a Comment