MWIMBAJI nyota wa muziki wa taarab nchini, Isha Ramadhani ‘Mashauzi’ ameamua kuvunjika ukimya kwa kusema bado ni mwimbaji halali wa kundi la Jahazi.
Isha ameelezea msimamo wake huo baada ya kuwepo na uvumi kwamba, ameamua kujiengua Jahazi na kuunda kundi lake akishirikiana na mama yake mzazi, Rukia.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Isha alisema bado hajafikiria kuhama katika kundi la Jahazi, linaloongozwa na Mzee Yussuf.
"Sio kweli, sijahama Jahazi, mimi bado ni mwimbaji halali wa kundi hilo na wala sijafikiria kabisa kuhama kwa sasa,”alisema mwimbaji huyo mwenye makeke.
“Isipokuwa baadhi ya siku huwa najumuika na wasanii mbalimbali kwa ajili ya kufanya maonyesho. Nadhani ndiyo sababu baadhi ya watu wakiniona, wanadai nimehama kwenye kundi langu," aliongeza.
Isha alikiri kuwa, ni kweli hakusafiri na kundi hilo hivi karibuni katika ziara yake ya mikoani kutokana na matatizo binafsi ya kifamilia na kwamba aliomba ruhusa kwa uongozi.
Akizungumzia matarajio yake ya baadaye, Isha alisema amepania kuwa msanii wa kimataifa wa muziki huo na kuongeza kuwa, amejipanga vyema kukamilisha ndoto hiyo.

No comments:
Post a Comment