Na Aboud Mahmoud, Zanzibar
FILAMU 81 kutoka nchi mbalimbali duniani zinatarajiwa kuonyeshwa wakati wa Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi Zanzibar (ZIFF) linalotarajiwa kuanza kurindima Juni 11 hadi 18 mwaka huu mjini hapa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, Mratibu wa Filamu wa ZIFF, Daniel Nyalusi alisema miongoni mwa filamu hizo, zipo 11 zilizotengenezwa hapa nchini.
Alizitaja baadhi ya filamu zitakazoonyeshwa katika tamasha hilo kuwa ni The rugged priest (Kenya), The rice paddy (China),The Crocodies (Sweden), The way home cinema (India) na Just an hour ago (Iran).
Zingine ni A hand full of dirt (Barbados), Making the bird (Uganda), Fambul tok (USA), Ni wakati (Kenya), Rebellion at down (Argentina), Lezare (Ethiopia), Orange (Namibia),Arapha(Italy).
Mratibu huyo alizitaja baadhi ya filamu zilizotengenezwa nchini kuwa ni Glamour, Manzese, Nazaeeli, Hotel less na Spicy voice.
"Filamu za mwaka huu ni nzuri sana na tunatarajia kuwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi,”alisema.
No comments:
Post a Comment