Vijana Stars
TIMU ya soka ya Taifa ya Uganda ya vijana wa chini ya miaka 23, The Cobs inatarajiwa kuwasili nchini kesho jioni.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema jana kuwa, timu hiyo itawasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere saa 10.30 jioni kwa ndege ya Uganda Air.
Wambura alisema msafara wa timu hiyo utaongozwa na Ofisa wa Shirikisho la Vyama vya Soka vya Uganda (FUFA), Sam Lwere.
Kwa mujibu wa Wambura, wachezaji na viongozi wa timu hiyo wamepangiwa kukaa kwenye hoteli ya Durban, iliyopo barabara ya Uhuru, Dar es Salaam.
The Cobs inatarajiwa kurudiana na timu ya Taifa ya vijana wa umri huo ya Tanzania, Vijana Stars, Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika pambano la marudiano la michuano ya Michezo ya Afrika.
Katika mechi ya awali, iliyochezwa wiki mbili zilizopita mjini Kampala, The Cobs iliichapa Vijana Stars mabao 2-1.
Ili Vijana Stars isonge mbele katika michuano hiyo, italazimika kuishinda The Cobs bao 1-0.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 1,000 kwa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa. Kwa upande wa VIP C na B, kiingilio kitakuwa sh. 5,000 na sh. 10,000 kwa VIP A. Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa keshokatika vituo vya Premier Betting (Kariakoo- mtaa wa Sukuma, Buguruni Sokoni, Manzese Midizini, JM Mall na Tandale kwa Mtogole), Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Steers (mtaa wa Ohio na Samora), Big Bon Msimbazi (Kariakoo) na Uwanja wa Uhuru.

No comments:
Post a Comment