MWIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amesema anatarajia kumtumia mcheza sinema, Ramsey Nouah kutoka Nigeria katika filamu yake mpya itakayojulikana kwa jina la Devil Kingdom.
Kanumba amesema kupitia tovuti yake juzi kuwa, ameamua kumtumia Ramsey, kufuatia kura zilizopigwa na mashabiki wake.
Mwigizaji huyo mwenye mvuto alisema, alitoa nafasi kwa mashabiki wake kumchagua mmoja wa wacheza sinema watatu kutoka Nigeria, ili afanye naye kazi nchini.
Mbali na Ramsey, wacheza sinema wengine aliowapendekeza ni Desmond Elliot na Van Vicker.
Katika kura hizo, ambazo hakutaja idadi yake, Kanumba alisema nyingi zilimchagua Ramsey na kupendekeza filamu hiyo iwe katika lugha mchanganyiko (kiswahili na kiingereza).
Kanumba alisema filamu anayotarajia kuicheza na Ramsey inahusu masuala ya jamii fulani, ambayo haiamini Mungu bali shetani na wamefanikiwa kuiteka dunia kwa nguvu za giza, pesa na umaarufu.
Mbali na kuiteka dunia kwa njia hizo, Kanumba alisema jamii hiyo pia inawasiliana kwa kutumia ishara maalumu na inafanya ibada kwa utaratibu iliojiwekea.
Kanumba alisema uamuzi wa kuwashirikisha wasanii kutoka nje katika baadhi ya filamu zake, umelenga kupanua soko lake kimataifa. Alisema filamu hiyo itatayarishwa kupitia kampuni yake ya Kanumba Great Film.
Kwa mujibu wa Kanumba, tayari Ramsey ameshawasili nchini kwa ajili ya kupiga picha za filamu hiyo, ambayo ipo kwenye hatua za mwisho.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi mjini Dar es Salaam, Ramsey alisema amefurahi kushirikishwa kwenye filamu hiyo na anaamini ushiriki wake utakuwa chachu.

No comments:
Post a Comment