YANGA imetoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya wageni wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Singida United mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa wa Taifa Dar es salaam.
Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa kocha George Lwandamina kukutana na aliyekuwa kipenzi cha wanayanga Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye anakifundisha kikosi cha Singida United chenye maskini yake mkoani Singida.
Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kiungo Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko aliyefunga bao la kwanza kunako dakika ya tano kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya mshambuliaji mpya, Ibrahim Hajib kuangushwa umbali wa mita 25.
Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda kwa misimu yote miwili iliyopita, Dany Usengimana akaifungia Singida United bao la kusawazisha dakika ya nane akitumia vizuri makosa ya nabeki wa Yanga kuchanganyana.
Mshambuliaji Mzimbabwe, Simbarashe ‘Simba’ Nhivi Sithole akaifungia bao la pili Singida dakika ya 23 akitumia tena makosa ya safu ya ulinzi ya Yanga.
Kipindi cha pili, kocha Mzambia wa Yanga alibadilisha karibu kikosi kizima akimtoa hadi kipa Beno Kakolanya na kumuingiza Mcameroon, Yoouth Rostand.
Mabadliko hayo yaliisaidia Yanga kupata mabao mawili dakika za mwishoni, akianza Mrundi Tambwe kusawazisha kwa penalti dakika ya 83 baada ya kipa Said Lubawa kumchezea rafu kiungo chipukizi, Said Juma, kabla ya Martin kufunga la ushindi dakika ya 90
No comments:
Post a Comment