KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, March 29, 2015

STARS, MALAWI DIMBANI LEO



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo inajitupa dimbani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, kumenyana na tmu ya taifa ya Malawi (The Flames), kuanzia saa
10.30 jioni.

Tiketi za mchezo huo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo vya uwanja wa Nyamagana na Uwanja wa CCM Kirumba, kwa bei za sh. 5,000 kwa mzunguko, sh. 12,000 kwa jukwaa kuu na sh.20,000 kwa viti vya jukwaa kuu maalumu.

Taifa Stars inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika wakiwa nafasi ya 91 kwenye viwango hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba, Mwanza, Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri , na kilichobakia ni mchezo wenyewe wa leo.

Mayanga alisema vijana wake wote 22 waliopo kambini wapo fiti, wamefanya mazoezi kwa siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba, wapo kwenye ari na morali ya juu na kwamba kikubwa wanachosubiri ni kushuka dimbani kusaka ushindi.

Aidha, Mayanga amewaomba wapenzi wa mpira wa miguu waliopo jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa, kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo.

Tayari waamuzi na kamishina wa mchezo wameshawasili jijini Mwanza. Mwamuzi wa kati atakuw Munyazinza Gervais kutoka Rwanda, akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda), mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda). Mwamuzi wa akiba  ni Martin Saanya kutoka Morogoro huku na Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza kutoka Mwanza.

Wachezaji wa Taifa Stars waliopo Mwanza ni Aishi Manula, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Salim Mbonde, Haji Makame, Hassan Isihaka na Abdi Banda.

Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Haroun Chanongo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank Domayo, Said Ndemla, John Bocco, Juma Luizio, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.

Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) iliwasili Mwanza juzi saa sita mchana, ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo dhidi ya Taifa Stars.

Malawi imewasili ikiwa na kikosi chake kamili cha wachezaji 18 na kufikia katika hotel ya JB Belimonte, wakiwemo wachezaji saba wanaocheza soka ya kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.

Wachezaji wa kimataifa waliowasili ni nahodha Joseph Kamwendo (TP Mazembe -Congo DR), Chimango Kayira (Costal de Soul - Msumbiji), Frank Banda (HBC Songo - Msumbiji), Esau Kanyenda (Polokwane City - Afrika Kusini),  Harry Nyirenda (Black Leopards - Afrika Kusini), Limbikani Mzava (Celtic - Afrika Kusini) Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe)

Wegine ni McDonald Harawa (Hoyale FC), Richard Chipuwa (Wanderers), Lucky Malata (Silver), John Lanjesi (Civo), Francis Mulimbika (Wanderers), John Banda (Blue Eagle), Earnest Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle), Chikoti Chiriwa (Red Lions), Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support Ballaton).

Mkuu wa msafara ni Alexander Waya, Kocha Mkuu, Young Chimodzi, Kocha Msaidizi, Jack Chamangwana, Kocha wa makipa, Pillip Nyasulu, Daktari wa timu, Levison Mwale, Meneja wa timu, Frank Ndawa na Ofisa Habari, James Sangala.

No comments:

Post a Comment