KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, October 26, 2014

TEGETE AIPAISHA YANGA, MDUDU WA SARE AIANDAMA SIMBA, AZAM CHALI



MDUDU wa sare ameendelea kuiandama Simba baada ya kulazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 na Prisons katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.


Sare hiyo ni ya tano mfululizo kwa Simba tangu ligi hiyo ilipoanza na imeendelea kuifanya ishike nafasi za chini katika msimamo wa ligi hiyo, inayozishirikisha timu 14.

Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Emmanuel Okwi kwa mpira wa adhabu dakika ya nane kabla ya Hamisi Maingo kuisawazishia Prisons dakika ya 89 kutokana na uzembe wa kipa Peter Manyika.

Azam walichezea kichapo cha kwanza baada ya kupigwa bao 1-0 na JKT Ruvu katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Bao pekee na la ushindi la JKT Ruvu lilifungwa na Samuel Kamuntu dakika ya 44 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Jabir Azizi.

Timu kongwe ya Yanga ilitoka uwanjani na pointi zote tatu baada ya kuichapa Stand United mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Mshambuliaji Jerry Tegete aliibuka shujaa wa Yanga baada ya kuifungia mabao mawili kati ya matatu. Bao lingine lilifungwa na Genislon Santos Jaja.

Katika mechi zingine za ligi hiyo zilizochezwa jana, Mgambo JKT iliichapa Ndanda FC bao 1-0 mjini Lindi, Kagera Sugar ilitoka sare ya bao 1-1 na Coastal Union mjini Tanga wakati Ruvu Shooting iliichapa Polisi Moro bao 1-0.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo wakati Mbeya City itakapoikaribisha Mtibwa Sugar mjini Mbeya.

No comments:

Post a Comment