'
Sunday, April 27, 2014
MOGELLA, MZIBA WATEMBELEA KLINIKI YA AIRTEL RISING STARS
Wachezaji nyota wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars Zamoyoni Mogella na Abeid Mziba, wakisalimiana na washiriki wa kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars inayoendelea kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars Zamoyoni Mogella, akiongea na washiriki wa kliniki ya soka ya kimataifa ya Airtel Rising Stars wakati walipowatembelea kwenye kliniki hiyo inayofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex.
Shirikisho la mpira wa miguu nchi (TFF), imetakiwa kuhahakisha inawalea vijana waliopata nafasi ya kushiriki kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars ili waweze kulisadia taifa kwa hapo baadae.
Wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa Abeid Musiba na Zamoyoni Mogella walitoa kauli hiyo
kwenye uwanja wa Azam wa Complex jijini Dar es Salaam jana, alipokwenda kuwatembelea
washiriki wa kliniki ambayo ina washiriki 72 kutoka nchi 12 Barani Afrika huku Tanzania
ikiwakilishwa na washiriki 19.
‘Ninayo furaha kuona mwekezaji kama Airtel kwa kushirikiano na Klabu ya Manchester United
ya Uingereza, zimejitokesa kusaidia maendeleo ya soka, hatuna budi kuhakikisha vipaji hivi
vinaendelezwa pamoja na kukuzwa zaidi,’ alisema Mogella.
Mogella alisema kuwa hana uhakika serikali imeweza kutoa miundo mbinu inayowezesha
michezo kufanyika, hivyo jukumu la kuhakikisha vipaji na elimu wanayoipata vijana hawa inabaki
kwa TFF.
"Kwa siku za karibuni serikali imekuwa ikitoa mazingira kwa wawekezaji kama hawa ili waweze
kufanya kazi yao vizuri. Na kwa maana hiyo nayo watahamasika na kuwekeza zaidi kwenye sekta
za michezo. Wakati sisi tunacheza mambo kama hayo hayakuwepo," alisema Mziba.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Yanga Africans alisema Tanzania na hata baadhi ya
nchi za Afrika zilikuwa hazifanyi vizuri kwenye michuano ya kimataifa sio kwa sababu hazina
vijana wenye vipaji vya soka, bali ni kutoka na ukosefu wa programu madhubuti za kuendeleza
vijana ambao ndio muhimili wa maendeleo ya soka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment