'
Monday, July 3, 2017
MALINZI, MWESIGWA WARUDISHWA TENA RUMANDE
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga, wamerudishwa rumande hadi Julai 17, mwaka huu, upepelezi wa kesi yao utakapokamilika.
Malinzi na wenzake hao walipandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakitokea rumande, ambako walipelekwa Julai 29, mwaka huu,
Walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza, Malinzi na wenzake hao walisomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF, iliyoko katika Benki ya Stanbic, Dar es Salaam.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Wilbord Mashauri, aliwanyima dhamana baada ya kutokea mabishano ya kisheria ya mawakili wa utetezi dhidi ya mawakili wa upande wa serikali na akawapangia kufika tena mahakamani leo.
Hata hivyo, hali imeendeelea kuwa mbaya kwa Malinzi na wenzake, baada ya kunyimwa tena dhamana leo, ambapo wamerudishwa rumande.
Katika mashitaka hayo 28 waliyoshitakiwa, 25 yanamuhusu Malinzi, akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote watatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment