Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa timu ya Yanga pamoja na kituo maalumu cha Kukuza vipaji vya michezo. |
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji ameipatia klabu yake eneo la zaidi ya ekari 700 lilipo Geza Ulole, Kigamboni, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Kisasa.
Akiwa amewakilishwa na wasaidizi wake wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume akiwa ameambatana na Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay, Sizya Lyimo na Kaimu katibu mkuu Baraka Deusdedit.
Eneo hilo lililopewa jina la Kijiji cha Yanga, rasmi utafanyika ujenzi wa kijiji cha michezo cha yanga ambapo patakuwa na uwanja wa kisasa wa mazoezi, uwanja wa mechi, hosteli na kituo cha kukuza vipaji kwa vijana pamoja na Hospital na shule.
No comments:
Post a Comment