TIMU ya soka ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, itashuka dimbani leo kumenyana na Ethiopia, katika mechi ya kundi B, itakayochezwa mjini Jinja nchini Uganda.
Mechi hiyo itakuwa ya pili kwa Kilimanjaro Queens tangu michuano hiyo ilipoanza mwishoni mwa wiki iliyopita. Katika mechi yake ya kwanza, Kilimanjaro Queens iliinyuka Rwanda mabao 3-2.
Ushindi huo umeiwezesha Kilimanjaro Queens, inayofundishwa na Kocha Sebastian Nkoma, kujihakikishia kucheza hatua ya nusu fainali kutokana na kundi hilo kuwa na timu tatu.
Mabao ya Kilimanjaro Queens katika mechi hiyo yalifungwa na Asha Rashid 'Mwalala' dakika ya 11 na 65 na Stumai Abdalla dakika ya 28. Mabao ya Rwanda yalifungwa na Ibangarrue Marie na beki Amina Ally wa Bara aliyejifunga wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa.
Mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Rwanda na Ethiopia ilitarajiwa kuchezwa jana. Mechi za nusu fainali zimepangwa kuchezwa Septemba 18 wakati mechi ya fainali itachezwa Septemba 20, mwaka huu, ikitanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.

No comments:
Post a Comment