'
Sunday, March 27, 2016
TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KNVB
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeomboleza kifo cha gwiji wa soka duniani Johann Cruffy aliyefariki hivi karibuni kwa ugonjwa wa Saratani.
Katika taarifa aliyoituma kwa Rais wa Chama cha Soka cha Uholanzi, Rais wa TFF Jamal Malinzi amemwelezea Marehemu Cruyff kama gwiji aliyetoa mchango mkubwa kama mchezaji na kocha katika timu ya Taifa ya nchi yake na klabu za Barcelona, Ajax, Lavanet mwaka 1964 – 1977.
Tanzania tulikuwa na bahati ya kutembelewa na Cruyff ikiwa ni sehemu ya kuitangaza klabu yake ya Barcelona na kuendeleza mpira wa Vijana na maendeleo ya walimu wa soka nchini.
TFF inaungana nawe, familia ya marehemu na wapenda soka ndani ya Uholanzi na duniani kote katika kuomboleza na kusheherekea maisha ya Marehemu Johann Cruyff. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amen.
Johann Cruyff alizaliwa Uholanzi tarehe 25 Aprili, 1947 na kuchezea klabu za Ajax, Feyenoord, Lavante, Los Angeles, Washington Diplomats na timu ya Taifa ya Uholanzi kati ya mwaka 1966 – 1977 na baadae alizifundisha kalbu za Ajax, Barcelona na Catalonia.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment