'
Sunday, March 20, 2016
TAIFA STARS YAENDA CHAD KWA MAFUNGU
KUNDI la kwanza la wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars) linaondoka leo kuelekea N'Djamena nchini Chad kwa ajili ya mechi ya kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mechi kati ya Chad na Taifa Stars itafanyika Jumatano Machi 23 mwaka huu na marudiano itacheza Machi 28 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili jana, kocha mkuu wa Taifa Stars, Boniface Mkwasa, alisema kuwa uamuzi wa kuondoka kwa 'mafungu' umetokana na baadhi ya wachezaji walioitwa kwenye timu hiyo kuwa na majukumu ya klabu nje ya Dar es Salaam.
Mkwasa alisema kuwa wachezaji wanaocheza nje ya nchi nahodha Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wataungana na timu hiyo huko huko N'Djamena.
"Tumefanya hivi ili kupata nafasi angalau ya kufanya mazoezi kwa siku tatu tukiwa huko huko Chad, ratiba ya Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho imetubana makocha wa timu za taifa safari hii, tutakutana na wachezaji muda mfupi kabla ya mechi," alisema Mkwasa.
Kocha huyo aliongeza kwamba licha ya changamoto hiyo, bado Taifa Stars ina nafasi ya kuanza vyema kampeni hizo kwa sababu alikuwa akifanya mawasiliano na wachezaji kwa ajili ya kuwaandaa na mchezo huo wa ushindani.
Stars itafanyika Jumatano Machi 23 mwaka huu na marudiano itacheza Machi 28 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
CHANZO CHA HABARI: NIPASHE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment