'
Sunday, February 1, 2015
WAANGALIZI WA SIRI KUSIMAMIA MECHI ZA MWISHO FDL
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litatuma waangalizi wa siri kwenye mechi za raundi ya 21 na 22 ambazo ni za mwisho kwa makundi yote ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zitakazoanza kuchezwa Februari 10 mwaka huu.
Mwangalizi huyo (match assessor) atatumwa na Katibu Mkuu ambapo baada ya mechi atatuma ripoti kwake kwa hatua zaidi.
Mechi za raundi ya 21 kundi A zitachezwa Februari 10 mwaka huu kati ya KMC na African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani), Kurugenzi FC na African Sports (Uwanja wa Mufindi), Majimaji na JKT Mlale (Uwanja wa Majimaji), Kimondo FC na Friends Rangers (CCM Vwawa, Mbozi), Ashanti United na Villa Squad (Uwanja wa Karume) na Polisi Dar na Lipuli FC (Uwanja wa Azam Complex).
Raundi ya 22 itachezwa Februari 16 mwaka huu kwa kuzikutanisha African Lyon na Polisi Dar (Uwanja wa Karume), Kurugenzi na Lipuli FC (Uwanja wa Mufindi), Kimondo FC na Majimaji (CCM Vwawa, Mbozi), JKT Mlale na Ashanti United (Uwanja wa Majimaji), Friends Rangers na African Sports (Uwanja wa Taifa), na Villa Squad na KMC (Uwanja wa Azam Complex).
Kundi B raundi ya 21 ni Februari 17 mwaka huu kati ya Burkina Faso na JKT Kanembwa (Uwanja wa Jamhuri), Mwadui na Polisi Tabora (Uwanja wa Mwadui), Polisi Dodoma na Green Warriors (Uwanja wa Jamhuri), Rhino Rangers na JKT Oljoro (Ali Hassan Mwinyi), Panone na Polisi Mara (Uwanja wa Ushirika), Geita Gold na Toto Africans FC (Geita).
Februari 22 mwaka huu ni JKT Kanembwa na Green Warriors (Lake Tanganyika), Mwadui na Burkina Faso (Mwadui), Polisi Tabora na JKT Oljoro (Ali Hassan Mwinyi), Polisi Dodoma na Panone (Uwanja wa Jamhuri), Toto Africans na Rhino Rangers (CCM Kirumba) na Geita Gold na Polisi Mara (Geita).
Mechi za viporo za Polisi Mara zitachezwa Februri Mosi dhidi ya JKT Kanembwa, na Februari 5 mwaka huu dhidi ya Polisi Tabora. Mechi zote zitachezwa kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment