'
Tuesday, February 10, 2015
KIONGOZI VILLA SQUAD APIGWA FAINI 600,000/-
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini ya sh. 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Villa Squad, Mbarouk Kassanda kwa kuhusika na uhamisho wa mchezaji Omari Ramadhan ambao haukufuata kanuni za usajili.
Villa Squad iliingiza majina tofauti ya mchezaji huyo wa African Lyon, ambapo badala ya Omari Ramadhan ikaingiza Omari Issa Ibrahim'. Kamati imeona Villa Squad ilifanya hivyo ili kudanganya, kuwezesha mfumo wa usajili wa kielektroniki ukubali jina la mchezaji.
Malalamiko ya kutaka kupewa pointi tatu na mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Villa Squad kwa kumchezesha mchezaji huyo, yametupwa na Kamati kwa sababu alikuwa ni mchezaji halali aliyethibitishwa (eligible) na TFF.
Kamati ilimuita mchezaji huyo na kumhoji kama alishiriki au alifahamu udanganyifu wa kubadili majina ili aweze kuingizwa katika mfumo wa eletroniki wa usajili lilibaki kuwa suala la mashaka. Inawezakana alishiriki au hakushiriki; Kamati haikupata ushahidi thabiti. Hivyo, Kamati iliamua kumpa mchezaji faida ya mashaka (benefit of doubts) na hivyo kutompa adhabu yoyote.
Kassanda ameadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) wakati Omari Ramadhan ni mchezaji wa African Lyon kwa vile ana mkataba na klabu hiyo.
JKT MLALE YATAKIWA KUILIPA LYON
Klabu ya JKT Mlale imeamriwa kuilipa African Lyon jumla ya sh. 600,000 ikiwa ni ada ya uhamisho na fidia kwa kumtumia mchezaji Noel Lucas kinyume cha taratibu kwenye mechi.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji baada ya kusikiliza malalamiko ya African Lyon ambapo ilibaini kuwa klabu hiyo ilikubali kulipwa sh. 300,000 ilikwa ni ada ya uhamisho.
Kamati imekataa maombi ya African Lyon kutaka pointi tatu na mabao matatu katika mechi yao ambapo Noel Lucas alicheza, kwa vile mchezaji huyo usajili huo ulithibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Pia JKT Mlale imetakiwa kuilipa African Lyon sh. 300,000 nyingine za usumbufu wa kufuatilia malipo ya mchezaji huyo. JKT Mlale imetakiwa kulipa fedha hizo kabla ya mechi yake ya mwisho ya ligi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment