KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, September 9, 2014

TAIFA STARS YACHAPWA 2-0 NA BURUNDI


TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars bado haijapata dawa ya kufuta uteja kwa Burundi baada ya kukandikwa mabao 2-0 katika mechi ya marudiano ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa jijini Bujumbura Burundi.


Stars iliyokwenda Burundi ikitamba kwenda kulipa kisasi cha mabao 3-0 ilichopewa na wenyeji wao kwenye mechi ya kirafiki ya kuadhimisha Siku ya Uhuru, ilishindwa kutimiza tambo hizo kwa kukandikwa na wenyeo wao kwenye mechi hiyo ya ugenini.

Mabao yaliyoizamisha Stars yalifungwa katika dakika ya kwanza tu ya mchezo na Saido Ntibazonkiza kabla ya Yusuf Ndikumana kuongeza la pili kwenye dakika ya 29 na kuifanya Stars ipigane kusaka angalau bao la kufutia machozi bila mafanikio yoyote.

No comments:

Post a Comment