Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa leo Novemba 04, 2016 ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri wiki ijayo kwenda Harare, Zimbabwe kucheza na wenyeji kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.
Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Novemba 07, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kikosi hicho siku inayofuata ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako itakuwa funga dimba la duru la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.
Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni:
Makipa
Deogratius Munishi –Young Africans
Said Kipao –JKT Ruvu
Aishi Manula –Azam FC
Mabeki
Erasto Nyoni -Azam FC
Michael Aidan -JKT Ruvu
Mwinyi Haji -Young Africans
Mohamed Hussein –Simba SC
David Mwantika -Azam FC
James Josephat –Tanzania Prisons
Vicent Andrew -Young Africans
Viungo wa Kati
Himid Mao -Azam FC
Mohammed Ibrahim –Simba SC
Jonas Mkude –Simba SC
Muzamiru Yassin –Simba SC
Viungo wa Pembeni
Abdulrahman Mussa -Ruvu Shooting
Shiza Kichuy –Simba SC
Simon Msuva -Young Africans
Jamal Mnyate –Simba
Washambuliaji
Ibrahim Ajib –Simba SC
John Bocco -Azam FC
Mbwana Samatta -K.R.C Genk ya Ubelgiji
Elius Maguli –Oman
Thomas Ulimwengu –Mchezaji huru
Omar Mponda -Ndanda
Kwa sababu mbalimbali hususani majeruhi, Mkwasa amewaacha wachezaji Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Kabunda (Mwadui FC), Juma Abdul na Juma Mahadhi wa Young Africans.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Harare, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zimbamwe liliomba TFF mchezo huo, nasi mara moja tukakubali.
Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kuna alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.
Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 144 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Zimbambwe yenyewe inashika nafasi ya 110.
Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Chile, Colombia na Ujerumani.
Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 31 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Senegal (32), Algeria (35), Tunisia (38) na Ghana (45).
Wachezaji wa Zimbabwe watakaochuana na Tanzania ni makipa: Tatenda Mukuruva (Dynamos) na Donovan Bernard (How Mine).
Mabeki: Godknows Murwira (Dynamos), Hardlife Zvirekwi (CAPS United), Ronald Pfumbidzai (CAPS United), Honest Moyo (Highlanders), Lawrence Mhlanga (Chicken Inn) na Teenage Hadebe (Chicken Inn).
Viungo: Tendai Ndlovu (Highlanders), Farai Madhanhanga (Harare City), Jameson Mukombwe (Chapungu), Tafadzwa Kutinyu (Chicken Inn), Ronald Chitiyo (Harare City), Talent Chawapihwa (ZPC Kariba) na Malvern Gaki (Triangle).
Washambuliaji: Pritchard Mpelele (Hwange), Gift Mbweti (Hwange), Leonard Tsipa (CAPS United), Rodreck Mutuma (Dynamos) na William Manondo (Harare City)
No comments:
Post a Comment