Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi akizungumza na wananchi pamoja na wasanii mbalimbali (hawapo pichani) wakati alipokua anafunga Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilioandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Wilayani Bagamoyo Oktoba mosi.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbet Makoye akitoa hotuba kwa wananchi pamoja na wasanii mbalimbali (hawapo pichani) wakati Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilioandaliwa na Taasisi hiyo lilipofungwa rasmi Wilayani Bagamoyo Oktoba mosi.
Vikundi mbalimbali vya burudani kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) vikitoa burudani kwa wananchi pamoja na wasanii mbalimbali (hawapo pichani) katika ufungaji wa Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilioandaliwa na Taasisi hiyo Wilayani Bagamoyo Oktoba mosi.
Baadhi ya wanachi walioshiriki ufungaji wa Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilioandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Wilayani Bagamoyo Oktoba mosi.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Katika kuhakikisha Watanzania wanafanya kazi kwa maendeleo yao na Taifa nchini Serikali imewataka wasanii mbalimbali kutumia Sanaa yao kuelimisha jamii umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii.
Wito huo umetolewa jana Wilayani Bagamoyo na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel katika hotuba yake ya kufunga Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lililoandaliwa na Taasisi ya Sanaana Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Katibu Mkuu katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa ya Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi amesema kuwa Wasanii wana nafasi kubwa ya kufikia Watanzania wengi kutokana na kazi zao hivyo watumie nafasi hiyo kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa Kufanya kazi.
“Wasanii mkidhamiria jambo hufanyika na uwezo wa kufanya hivyo mnao,ni vizuri mkatumia Sanaa yenu kuwaelimisha wanachi manufaa ya kufanya kazi kwao wenyewe na Taifa kwa ujumla”.Alisema Prof.Ole Gabriel.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbet Makoye mbali na kuwashukuru wasanii wote waliohudhuria Tamasha hilo amewataka pia waendelee kufanya Sanaa zenye ubora na zinazoitangaza Tanzania Ulimwenguni.
“Mmeshiriki vizuri katika Tamasha hili niwasihi muendelee kufanya Sanaa iliyo bora inayotangaza nchi yetu kote Ulimwenguni ukizingatia tunazo Sanaa za aina mbalimbali ikiwemo ngoma,muziki,filamu na sanaa za ufundi”.Aliongeza Dkt.Makoye.
Aidha msanii Ebeneza Lukas anaefanya muziki amesemaTamasha limempa ujuzi na weledi mkubwa katika Sanaa yake ukizingatia kuwa yeye ndio anaanza kufanya Sanaa.
Tamasha hilo lililofunguliwa Septemba 26 mwaka huu na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa naMichezo Mhe.Anastazia Wambura limefungwa Oktoba mosi ambapo kazi mbalimbali za Sanaa zilifanyika ikiwa ni pamoja na makongamano na warsha mbalimbali.

No comments:
Post a Comment